1 Chronicles 6

Wana Wa Lawi


1 aWana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.

2 Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

3 bAmramu alikuwa na wana:
Haruni, Musa, na Miriamu.
Haruni alikuwa na wana:
Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

4 Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua,

5 Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi,

6 Uzi akamzaa Zerahia,
Zerahia akamzaa Merayothi,

7 Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,

8 cAhitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi,

9 Ahimaasi akamzaa Azaria,
Azaria akamzaa Yohanani,
10 dYohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Sulemani huko Yerusalemu),

11 eAzaria akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,

12 Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Shalumu,

13 fShalumu akamzaa Hilkia,
Hilkia akamzaa Azaria,

14 gAzaria akamzaa Seraya,
Seraya akamzaa Yehosadaki.

15 hYehosadaki alihamishwa wakati Bwana aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.


16 iWana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.

17 Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:
Libni na Shimei.

18 Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

19 jWana wa Merari walikuwa:
Mahli na Mushi.

Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao:

20 Wazao wa Gershoni:
Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi,
Yahathi akamzaa Zima,
21 kZima akamzaa Yoa,
Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera,
Zera akamzaa Yeatherai.

22 lWazao wa Kohathi:
Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora,
Kora akamzaa Asiri,
23Asiri akamzaa Elikana,
Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,

24 mAsiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,
Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.

25 Wazao wa Elikana walikuwa:
Amasai na Ahimothi,

26 Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai,
Sofai akamzaa Nahathi,
27 nNahathi akamzaa Eliabu,
Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana,
Elikana akamzaa Samweli.

28 oWana wa Samweli walikuwa:
Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,
na Abiya mwanawe wa pili.

29 Wafuatao ndio wazao wa Merari:
Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,
Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

30 Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,
Hagia akamzaa Asaya.

Waimbaji Wa Hekalu

31 pHawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

33 qWafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao: Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,

34 rmwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,
mwana wa Elieli, mwana wa Toa,

35 mwana wa Sufu, mwana wa Elikana,
mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,

36 mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli,
mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

37 smwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,
mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

38 tmwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,
mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;

39 una msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:
Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,

40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,
mwana wa Malkiya,
41mwana wa Ethni,
mwana wa Zera, mwana wa Adaya,

42 mwana wa Ethani, mwana wa Zima,
mwana wa Shimei,
43mwana wa Yahathi,
mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

44 Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:
Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi,
mwana wa Maluki,
45mwana wa Hashabia,
mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,

46 mwana wa Amsi, mwana wa Bani,
mwana wa Shemeri,
47mwana wa Mahli,
mwana wa Mushi, mwana wa Merari,
mwana wa Lawi.

48 vNdugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. 49 wLakini Haruni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Musa mtumishi wa Mungu.


50 xHawa ndio waliokuwa wazao wa Haruni:
Haruni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua,
51Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,

52 Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,
53 yAhitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi.

54 zZifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Haruni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): 55 aaWalipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka. 56 abLakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
57 acKwa hiyo wazao wa Haruni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, 58 adHileni, Debiri, 59 aeAshani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho.
60 afKutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.
Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.

61Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

62Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

63 agWazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

64 ahKwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho. 65Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

66Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu. 67 aiKatika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, 68 ajYokmeamu, Beth-Horoni, 69 akAiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.

70 Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.


71 alWagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:
Katika nusu ya kabila la Manase:
walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.

72 amKutoka kabila la Isakari
walipokea Kedeshi, Daberathi,
73Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

74 anKutoka kabila la Asheri
walipokea Mashali, Abdoni,
75 aoHukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

76 Kutoka kabila la Naftali
walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.


77 Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:
kutoka kabila la Zabuloni
walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.

78 apKutoka kabila la Reubeni, ng’ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko
walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa,
79 aqKedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.

80 arNa kutoka kabila la Gadi
walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu,
81 asHeshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.
Copyright information for SwhKC